Mama yake Dogo Janja awa hoi baada ya kukabidhiwa

Jumatano , 5th Dec , 2018

Msanii wa Bongofleva Dogo Janja a.k.a 'Janjaro', amesema baada ya kumkabidhi mama yake nyumba mpya na kumtoa kwenye maisha ya kupanga aliishiwa nguvu na hajasema lolote zaidi ya kila muda kuonekana haamini kilichotokea.

Nyumba ambayo Dogo Janja amemkabidhi Mama yake. picha ndogo ni Dogo Janja akiwa na mama yake.

Akiongea na www.eatv.tv leo Dogo Janja amesema aliamua kuvaa jukumu la kuwa baba na kupeleka faraja kwa mama yake mzazi baada ya baba yake kufariki miaka miwili iliyopita.

''Ninafurahi nimekamilisha hili ndani ya miaka miwili, nilijjiwekea malengo haya baada ya kufariki kwa baba yangu ambaye daima alikuwa ananisisitiza niwekeze kwenye mali kama ardhi na nyumba, sasa nimemfurahisha mama yangu kiasi kwamba amekosa cha kusema yaani yuko “Too Emotional”, amesema Janjaro.

Dongo Janja amefunguka kuwa yeye aliondoka nyumbani akawaacha wazazi wake wakiwa kwenye nyumba ya kupanga na muda wote alikuwa analala sebuleni lakini leo ametimiza ndoto kubwa ya kuwa na kwao hivyo mama yake ana haki ya kufurahi.

''Mama ana kila sababu ya kufurahi natamani hata baba angekuwepo yeye alikuwa mshauri wangu mkuu lakini hayupo tena tutaendelea kufanya dua tu kwaajili yake maana ndicho anachostahili kwasasa, huwezi kusema utampa pesa au mali'', ameongeza.