''Hainaga Ushemeji ni ngoma iliyokuwa Offcial kutambulisha mziki wa Singeli na sitokuja kutoa ngoma kubwa kama Hainaga Ushemeji''
Manfongo ameongeza kuwa wakati anaandika nyimbo ya Hainaga Ushemeji alikuwa anatafuta brand yake na kutaka watu wamfahamu kwamba yeye ni nani katika mziki wa singeli ndiyo maana aliandika ngoma hiyo ambayo ilimpa mafanikio makubwa.
Hata hivyo Manfongo amesema wimbo wake huo haukumsaidia yeye peke yake kutambulika na kupata maendeleo bali anakiri kwamba wimbo huo uliweza kusaidia mziki wa singeli kutambulika na kuwa mziki wa biashara na mpaka sasa wasanii wa Singeli wanalipwa vizuri wanapoitwa kwenye show.
Manfongo amemalizia kwa kusema kuwa ataendelea kuandika nyimbo nyingine nyingi lakini hana imani ya kuandika nyimbo kubwa kama Hainaga Ushemeji kwani kwa chochote atakachofanya watu wataona hajafikia ngoma hiyo.
