Jumatatu , 26th Apr , 2021

Msanii wa BongoFleva Ally Nipishe amefunguka kusema mapenzi yamemtesa na yamemrudisha nyuma kupata mafanikio kutokana na mtu aliyekuwa naye kwenye mahusiano.

Msanii Ally Nipishe

Ally Nipishe amesema watu wasiwashangae wasanii kuimba nyimbo za mapenzi kwani hata wao wenyewe yanawatesa japo mashabiki hawajui kitu gani kinawatokea na kinachoendelea kwao.

"Mapenzi yamenitesa na yananikumbusha mbali mpaka natamani kulia, yaliniyumbisha sana kwenye 'game' kwa sababu kipindi kile nilikuwa naanza kufanikiwa halafu mtu anakuja kunirudisha nyuma, hakuna mtu anaeweza kuyamudu mapenzi ila watu wana-maintain tu" amesema Ally Nipishe

Mengine zaidi aliyoyazungumza Ally Nipishe kuhusu kuteswa na mapenzi bonyeza hapa chini kutazama.