"Mara ya pili sasa mnaniua" - Hussein Machozi

Alhamisi , 26th Mar , 2020

Msanii Hussein Machozi amefunguka kusema watu wanatamani afariki kweli au la maana  anazushiwa kifo kwa mara ya pili sasa kupitia chombo kimoja cha habari ambacho kilitangaza kifo chake kupitia mtandao wa Youtube.

Msanii Hussein Machozi

Hussein Machozi amesikitishwa na taarifa hizo ambapo amesema yeye ni mzima wa afya, yupo salama na kama kuna kosa alilowahi kufanya basi awaombe watu msamaha ili mradi wasimzushie taarifa hizo tena.

Kupitia akaunti yake ya mtandao wa Instagram Hussein Machozi ameeleza kuwa,  

"Kah jamani mbona mnaniua namna hii, hata kama hamnipendi sio hivi asee mimi nipo salama tena nina afya tele, msinifanyie hivi  jamani  kwani niliwakoseaga nini  mniambie basi niwaombe msamaha maana mara ya pili sasa mnaniua, ama mnataka nidedi kweli" ameandika Hussein Machoz