MC Pilipili ajibu suala la mkewe kuwa mkuregenzi

Jumamosi , 11th Jan , 2020

Mchekeshaji na mshereheshaji MC Pilipili amefunguka kusema suala la mke wake Qute Mena, kukosa kazi sio la ukweli kwa sababu sasa hivi ni mkurugenzi wa shule za awali.

Pichani ni Mc Pilipili na mkewe Qute Mena

Mc Pilipili amesema hivyo kupitia EATV & EA Radio Digital, baada ya kuwepo na taarifa zinazosema mke wake hana kazi ya maana hapa mjini na huwa anasafiri naye kila mahali.

"Hapana, mke wangu napata nafasi ya kusafiri naye kwenye  muda wa likizo hivi na mimi ndiyo naamua, mke wangu sasa hivi ni mkurugenzi na msimamizi wa shule ya awali, kwa wanavyosema kwamba hana kazi wasidhani ni lazima awe anafanya ninachokifanya mimi, lakini mke anatakiwa aonekane kwenye kazi ambayo mimi naifanya" ameeleza Mc Pilipili.

Aidha Mc Pilipili ameendelea kusema "Mke wangu yupo vizuri, yupo poa na ana kazi yake ambayo anaifanya, wanavyosema kwamba hana kazi nachukulia kama ni maoni ya watu wanayotoa na mimi naheshimu mawazo yao kwamba wakisema mke wangu yupo hivi ama  vile". ameongeza