Mfahamu kiundani Jaguar Paw

Jumatatu , 12th Feb , 2018

Anafahamika maarufu kwa jina la Jaguar Paw, lakini jina lake halisi ni Rudy Youngblood. Alizaliwa September 21, 1982 huko Belton, Texas lakini ni 'Native American'.

Rudy ana wadogo zake wa kike wawili ambao amekuwa nao wakilelewa na mama yao, akiwa na miaka 10 alianza kufanya kazi katika sites za ujenzi kama vibarua na kujifunza kazi zingine za kiume, kama useremala, kutengeneza matofali na nyinginezo.

Rudy alikuwa akisoma katika shule za kawaida za umma maarufu kama Kayumba huku kwetu bongo. Alikuwa akipenda sana mchezo wa ngumi na kutazama filamu. Familia yake ilitamani sana ahitimu high school, na alipomaliza alipata scholarship katika vyuo vikubwa vya sanaa, akini hakwenda huko na kuamua kuingia katika ngoma za asili, na kupata fursa ya kuperform katika tamasha kubwa la ngoma za asili za Wamarekani wenye asili ya India ( Red Indians).

Mwaka 2006 alipata dili la kuigiza filamu ya Apocalypto kama Jaguar Paw, kijana kutoka jamii ya Mayan anayeteta watu wake dhidi utawala mbovu, iliyotengenezwa na mtayariushaji maarufu wa filamu duniani, Mel Gibson na kumpa umaarufu mkubwa, ingawa haikuwa filamu yake ya kwanza.

Tazama orodha ya filamu alizoigiza

2005Spirit: The Seventh FireWarrior Protector

2006ApocalyptoJaguar Paw

2010BeatdownBrandon Becker

2012Into the AmericasToowin

2015WindwalkersMatty Kingston

2016Crossing PointMateo