Jumanne , 30th Mei , 2017

Nyota wa muziki wa bongo fleva Msami anayehit na ngoma ya 'So Fine' amefunguka kwa kudai kuwa ubinafsi na kukosa ushirikiano miongoni mwa wasanii ni moja  kati ya sababu zinazowafanya ya wasanii wa muziki kushindwa kufanya vizuri kimataifa

Msami amefunguka hayo hivi karibuni kwa kudai kwamba muziki wa bongo kutopiga hatua zaidi kimataifa kumetokana na baadhi ya wasanii wanaofanya vizuri kimataifa kuwa wabinafsi kwa kushindwa kutoa nafasi  kwa wengine kuonekana.

“Kukosa ile roho ya kuwa na umoja na ukweli ndani ya nafsi yako. Tunafanya vitu vinakwama unaaza kujiuliza mwenyewe umekwama kwa sababu gani unagundua ninakosa ushirikiano, unarudi mwenyewe unanza kutengeneza ushirikiano na watu. Hata kama unataka kwenda kimataifa na huku ndani huna ushirikiano hata mashabiki nao watajigawa ndio unakuta wanapambana mtu fulani akose tuzo nje” - amesema Msami.