Ijumaa , 18th Jan , 2019

Mkali wa 'Hit song' za kitambo, P1 Black ambaye aliyetamba na ngoma kama 'Nini mnataka' na 'Nisikilize me' ft Mr blue amesema baada ya kimya kirefu sasa ameamua kurejea rasmi akiwa amelisoma vizuri soko la muziki na kujipanga.

P1 Black

P1 Black ambaye zamani alifahamika kama Pig Black amefunguka hilo kwenye Heshima ya Bongofleva ya Planet Bongo ya East Africa Radio ambapo amesema tayari amerekodi ngoma 20.

''Nimerejea na baada ya ngoma ya Kamshange itakuwa ni 'back to back' maana sijarekodi hizo ngoma 20 ili zikae ndani bali ziwafikie mashabiki'' - P1 Black.

Mkali huyo pia amefunguka kwamba kati ya ngoma hizo 20, 17 zimetengenezwa kwa MJ Records na producer Daxo Chali huku Mixing na Mastering ikifanywa na Marco Chali.

Ametaja sababu ya kufanya ngoma nyingi MJ Records ni kutokana ukongwe wa studio hizo ambapo imekuwa kama familia yake hivyo inampa uhuru wa kushughulika na mambo mengine kama video pale tu anapokuwa amemaliza kuingiza Vocal na kuwaachia MJ Records wakamilishe kazi yao.

Mkali huyo pia amesema ngoma hizo 20 zote ni hit kali kwani yeye mwenyewe ana sikio la muziki mzuri hivyo akimaliza kurekodi tu huwa anajua kama ngoma aliyorekodi ni kali.