
Picha ya pamoja Msanii Shilole na mumewe Rommy 3D
Maoni yamekuwa mengi baada ya performance yake siku ya jana kwenye kilele cha Wiki ya Wananchi baada ya kutumbuiza na mashabiki kupata nafasi ya kuuona muonekano wa mwili wake huku wengi wakishauri apungue.
“Woote wanaotaka mke wangu apungue hawaitakii mema ndoa yetu (ni wachawi) kwasababu kwenye historia yangu sijawahi kupenda dem kimbaumbau, napenda mabonge haswaaaa (wanaonijua wanajua)”.
Rommy 3D aliendelea kumtetea mke wake huyo kupitia instagram kwa kuandika “Mke wangu Shilole wasikudanganye endelea kunenepa mama, Nakupenda!!!”