Ijumaa , 3rd Jul , 2020

Tumezoea kuona wasanii maarufu kutaka kuwa viongozi hasa katika nyadhifa ya Ubunge ila hii ipo tofauti kwa msanii wa filamu Rado ambaye amesema anataka kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2025.

Msanii wa Filamu Rado

Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital msanii huyo wa filamu amesema mwaka huu alikuwa na mipango ya kugombea Urais wa Tanzania ila kwa sababu ya kazi anayoifanya Rais Magufuli ni kubwa na anatakiwa kuungwa mkono ila yeye atagombea 2025.

"Watu hawajui ndoto yangu kesho nataka kuwa nani, mwaka huu nilikuwa nategemea kugombea Urais wa Tanzania, ila kwa sababu kazi anayoifanya Rais Magufuli ni kubwa inatakiwa kupewa sapoti, kuungwa mkono, kushikwa mkono na kuheshimiwa, mimi nitasubiri hadi Rais wangu Dkt John Pombe Magufuli akimaliza muda wake mwaka 2025, na mimi ndiyo nitatia nia ya kugombea Urais" ameeleza msanii wa filamu Rado

Zaidi tazama kwenye mahojiano kamili hapa chini.