Ijumaa , 24th Jul , 2015

Star wa muziki Tanzania, Mwana FA ametoa somo kukumbusha wasanii wenzake kusuka kazi zao katika namna ya kuburudisha zaidi, hata kama rekodi zenyewe zinataka kufikisha ujumbe wa aina fulani mgumu katika jamii.

Star wa miondoko ya bongofleva nchini Mwana Fa akiwa na mastaa wenzake wa muziki

FA ambaye amemsifia sana Professa Jay kutokana na uwezo wake mkubwa katika hili, akitolea mfano wa ngoma kama Chemsha Bongo na Bongo Dar es Salaam, amesema hayo akigusia pia uhalisia wa maisha ya watu ambao kwa asilimia kubwa hutumia muziki kujiburudisha baada ya harakati.