Alhamisi , 11th Jun , 2015

Staa wa muziki Mwasiti Almasi, ameeleza mchango mkubwa wa staa wa muziki Chidi Benz katika kuikuza sanaa yake, kupitia rekodi ya 'hao' ambayo walifanya kwa kushirikiana.

msanii wa miondoko ya bongofleva Mwasiti Almasi akiwa na rapa Chidi Benz

Na hii ni kutokana na rapa huyo kufanikisha kufanyika kwa kazi hiyo licha ya mazingira magumu yaliyokuwepo kwa wakati huo.

Mwasiti amesema kuwa, kazi hiyo aliifanya mwaka 2007 lakini mpaka leo hawezi kusahau, kwa nafasi ya chini aliyokuwepo katika sanaa yake, na kiki ya juu ambayo Chidi alikuwa anaishikilia kwa upande wa rap kwa kipindi hicho, na hiki ndicho alichokieleza Mwasiti juu ya vile anavyomuelewa Chidi.