
Upande wa kulia ni kipa wa Simba Aishi Manula, kati Mzee wa Utopolo, na kushoto Haji Manara.
Kamera za EATV & EA Radio Digital imempata shabiki kindakindaki wa timu hiyo Mzee wa Utopolo ambaye amefunguka matarajio ya timu yake, pia amempa onyo kipa wa Simba Aishi Manula na msemaji wa timu hiyo Haji Manara juu ya uwezo wa mchezaji wao mpya Carlinhos.
"Historia ya mchezaji wetu Carlinhos inavyosemekana makipa wengi waliokuwa wanajaribu kufuata mipira yake wameishia Hospitali, ukijaribu kufuata mipira yake mikononi basi ujue viganja hauna, namuonya sana Aishi Manula akijaribu kufuata mipira ya huyu bwana basi ni Hospitali moja kwa moja" amesema Mzee wa Utopolo
Akizungumzia onyo lake kwa Haji Manara Mzee wa Utopolo ameongeza kusema "Ujumbe wangu kwa Manara namuomba jumapili akae kwenye station ashuhudie wananchi tunavyofaana, pia nampa onyo maana anavyoongea abakize maneno kwa sababu Oktoba hatuchezi Simba na Yanga tunacheza timu ya babu na wajukuu"
Zaidi tazama akijitamba hapa chini kwenye Video.