Jumatatu , 17th Jan , 2022

Rais wa kitaa Nay wa Mitego 'The Trueboy' amesema kuwa ame-miss ule ushindani wa kwenye muziki wa rap maana anajiona yeye tu kila kona kwenye nafasi hiyo.

Picha ya msanii Nay wa Mitego

"Wasanii wengine wa rap wapo wapi kwani mbona siwaoni, najiona mimi tu kila kila kona mtaani mpaka kwenye trending zao nipo mimi tu na hunijui, namiss ule ushindani kweli" ameandika Nay wa Mitego

Nay wa Mitego ameeleza hilo baada ya ngoma yake mpya ya hunijui kufanya vizuri kwenye TV, Radio na mitandao ya kijamii.