Nandy afunguka mapya kumuenzi Ruge

Jumamosi , 30th Mar , 2019

Msanii Nandy ambaye alikuwa ni mtu wa karibu wa marehemu Ruge Mutabahaba, kwa mara ya kwanza amefunguka juu ya kilichokuwa kikiendelea juu yake wakati wa msiba, ambacho kiliibua maswali mengi kwa jamii.

Akizungumzia hilo, Nandy amesema kwa sasa hadhani kama ni sahihi kujadili masuala yake binafsi, ila watu wanatakiwa wajue kuwa aliguswa na msiba kama watu wengine, na sasa msiba umekwisha, hivyo ni muda muafaka wa watu kuendelea kufanya yale aliyokuwa akiyapigania Ruge, ikiwemo kufanya kazi kwa bidii.

Nandy akisimulia kila kitu

“Msiba umegusa watu wengi sana, ni mtu ambaye anapenda kila mtu afanye kazi, ni mtu ambaye anapenda kuona mafanikio ya kila mtu, kwa hiyo tuko hapa kwa ajili ya kumfanya awe 'proud' na sio 'kumdissapoint'.

“Kila mtu ameumizwa na msiba kwa namna yake ya tofauti, sipendi sana kuongelea masuala ya msiba kwa sababu yameshapita, kwa yeyote aliyepokea kwa fikra yake kwa kipindi kile abaki na fikra yake, sasa hivi yameshasonga mbele na maisha mengi yanaendelea, marehemu alikuwa ni mtu ambaye anapenda kila mtu afanye kazi, ni mtu ambaye anapenda kuona mafanikio ya kila mtu, kwa hiyo tuko hapa kwa ajili ya kumfanya awe proud na sio kumdissapoint.”, amesema Nandy

Kutokana na hayo, Nandy amesema kwamba kwa sasa watu watarajie kazi bora zaidi kutoka kwake, huku akiwataka watu kutazama video yake mpya akiwa na msanii wa Kenya Willy Paul, inayoitwa Haleluya.