Kwenye Planet Bongo ya East Africa radio Nandy amesema kuwa miongoni ya wasanii wanaosapoti anachokifanya ni Dully Sykes na kwamba maneno ya mtaani ni ya kupuuzwa kwani hayana ukweli wowote.
“Dully yupo sana proud na mimi kila tukikutana huwa ananisisitiza kuwa na heshima, kusikiliza wakubwa walionitangulia, kufanya kazi kwa bidii kwa sababu hustling yangu aliiona toka way back na ndoto zangu anazijua nyingi sana,” Nandy alifunguka.

Aidha Nandy ameomgeza kwamba "Huniambia ndoto zako zimetimia, so usiachia hiyo chance kwako kwa kufanya lolote baya.” ameongeza.
