Ijumaa , 16th Dec , 2016

Albam ya wasanii Navy Kenzo ambayo inatarajiwa kutoka kabla ya mwezi huu kuisha, imehusisha wasanii mbalimbali wakiwemo wa ndani na nje ya Tanzania.

Cover ya albam mpya ya navy Kenzo

Wasanii hao ambao wameibuka washindi wa kundi bora kwenye EATV AWARDS, wametoa orodha ya wasanii walioshiriki kwenye albam hiyo, wakiwemo walioimba nao na wengine wakiwa miongoni mwa waliochangia uandishi wa nyimbo za kwenye albam hiyo.

Wasanii watakaosikika kwenye albam hiyo ni pamoja na Alikiba (Tanzania), Patoran King (Nigeria), Wild Dad (Tanzania) Mr. Eazi (Ghana), Dj Moshe Buskila (Israel), R2Bess (Ghana) na Rosa Ree (Tanzania).

Pia wasanii walioshiriki kuandika nyimbo za kwenye albam hiyo ni pamoja na wenyewe Navy Kenzo, Barnaba, Nikki wa Pili, G Nako, Rosa Ree, Wildad na Tay.

Albam hiyo imepikwa na producers tofauti tofauti wakiwemo Nahreel, Chopstix na Dj Moshe Buskila ambaye ni Muisrael, na amaemua kuifanyia ngoma ya 'feel good' remix huku akiwazawadia ngoma moja ya ziada baada ya wimbo wa 'feel good' kuwa hit, huku mastering na mixing ikifanywa na Chizan Brain.

Kwa hili Navy Kenzo wamekuwa na uthubutu wa kutoa albam wakati huu, kipindi ambacho wasanii wengi wanaogopa kwa kuhofia changamoto za wizi wa mtandaoni.