Jumatano , 31st Mei , 2017

Msanii Neddy Music anayefanya poa na ngoma ya 'Doze' amejibu kejeli ya  Dogo Janja kwamba hajui kuvaa kwa kusema kuwa msanii huyo hana adabu kwa watu wazima ndiyo maana ameweza hata kutoa kauli hiyo kwake ambaye ni kaka yake kwenye mitupio.

Nedy ametoa jibu hilo kwenye kipindi cha 5Selekt cha EATV kwa kusema kwamba Dogo janja kumfananisha na Mkongo kwenye suala la kuvaa ni kukosa adabu ndio maana hata alipojua amekosea akaanza kujitetea kwamba watu wanawapambanisha.

"Dogo Janja hana heshima ndiyo maana aliweza kuzungumza kauli ile, Naweza kumfananisha na kijana anayeweza kuwakuta wazee wamekaa bila  kusalimia alafu akauliza mbona hamjanisalimia wakati ni wajibu wake kuanza kuwasalimia . Sasa Janjaro ni mdogo wangu kwenye suala la mavazi. Mtu ambaye anawaza kukaa chini na kunipambanisha naye atakuwa ana matatizo ya akili na achunguzwe vizuri" - Neddy Music.

Pamoja na hayo Neddy ameweka wazi kwamba hana Matatizo yoyote na msanii huyo ambaye kwa sasa anasumbua masikio ya mashabiki zake inayokwenda kwa jina la 'Ukivaaje unapendeza' ndiyo maana hakutaka kubishana naye au kutengeneza bifu.