Nedy afunguka kuhusu kutapeli watu na kufumaniwa

Jumatatu , 9th Sep , 2019

Msanii Nedy Music amefunguka kuhusu malalamiko ya kutapeli watu pesa, kuomba picha za utupu wanawake katika mitandao ya kijamii pamoja 'issue' za kufumaniwa.

Nedy Music ameeleza hayo baada ya kupost picha ya malalamiko hayo na kuifuta katika mtandao wa kijamii wa Instagram siku kadhaa zilizopita.

Akiongea na EATV & EA Radio Digital Nedy Music amesema kuwa,

"Ni mtu ambaye alikuwa anatapeli watu Nedy feki, alikuwa anafanya hivyo kwa muda ila niliweza kumpata kumpeleka kituoni na alikiri hatarudia lakini baada ya muda alianza kurudia hayo mambo, kwa hiyo mitaani zilikuja stori kwamba Nedy anaomba watu pesa ya mafuta na studio".

Nedy Music ameendelea kusema alikuwa anapata maoni na kupokea meseji za watu kutaka pesa zao na aliamua kupost ili ajulishe watu kwamba hahusiki kwenye kutapeli watu wala kuomba picha za utupu.

Aidha msanii huyo amezungumzia endapo kama atakutwa na 'issue' za kufumaniwa ambapo amesema,

"Haitawahi kutokea na haitakuja katika maisha yangu kwa sababu mtu ambaye nipo naye ni tupo wawili tu hakuna mtu mwingine na siwezi kuwa na mahusiano na mwanamke wa mtu" amesema Nedy Music.