Alhamisi , 24th Dec , 2020

Staa wa filamu Elizabeth Michael ni mmoja kati ya wasanii ambao wanajibu sana 'comments' za mashabiki wake pale wanapo-comment kwenye picha au video anazp-post kwenye mitandao ya kijamii.

Msanii wa filamu Elizabeth Michael

Hilo limeendelea siku ya leo baada ya ku-post picha kwenye Instagram kisha mashabiki zake ku-comment kwenye picha hiyo, ila majibu aliyoyatoa yana ukakasi na kufanya watu kujiuliza ni picha au kuna kingine.

Shabiki wa kwanza ali-comment kuwa "Hivi ni nani alikuambia ukibadilisha rangi ya nguo hautapendeza maana kila siku ni gauni jekundu

Elizabeth Michael alimjibu shabiki huyo kwa kuandika "Kuna hela yako yoyote unachangia inakuuma labda tulia kama mpenzi mtazamaji bro, nikusaidie tu nyekundu ni rangi yangu pendwa

Shabiki alimchokoza kwa ku-comment kuwa "Umeona shepu mpya mjini ya mke mwenzio

Aidha msanii huyo hakumuacha salama alimrudia kwa kumjibu "Nina wake wenza kama 100 hivi, sasa sijajua ni yupi"