Jumatano , 22nd Jul , 2015

Wasanii wa kundi la 'Weusi' Joh Makini Nikki wa Pili na G Nako wametumia nafasi kufafanua juu ya rekodi yao mpya inayokwenda kwa jina 'Laini'

wasanii wa kundi la muziki la weusi nchini Tanzania

Baada ya kundi la Weusi siku ya jana kuibariki kampeni ya Zamu Yako 2015 kwa kuzindua ngoma maalum kwa ajili ya kampeni hiyo, kwa upande wa kazi zao binafsi wimbo huo unaoonesha pande mbili za muziki wanaoufanya na namna wanavyoweza kuumudu.

Niki ametumia mistari na ujumbe mwepesi, wakati G Nako akipita njia ngumu, falsafa ambayo pia inawasilishwa na 'kava' ya kazi yenyewe ikiwa inaonesha kofia ngumu na kofia ya kulia bata kama anavyofafanua msemaji wa kundi hilo, Nikki.

Kutokana na mafanikio ya rekodi ya 'Nusu Nusu' katika vituo vya kimataifa, Nikki wa Pili pamoja na G Nako anaelezea pia ujio wa video ya Laini.