Jumamosi , 31st Aug , 2019

Rapa Nikki Wa Pili ameeleza suala linalohusu watu katika utumiaji wa mitandao ya kijamii na ametaja watu wanaoongoza kuangalia video chafu mitandaoni.

Nikki Wa Pili

Nikki Wa Pili ameiambia EATV & EA Radio Digital, kuhusu kushambuliwa kwa kum-post mpenzi wake mara kwa mara katika mitandao ya kijamii.

"Huwezi kumuelezea mtu anayekushambulia, mitandao ya kijamii ni imetuonyesha tupo wapi katika uwezo wa kufikiri, pia imeonyesha jinsi gani watu wana chuki na wivu lakini wengi wamekuwa hawana maana, mimi huwa naangalia mtu anasema kitu gani cha maana".

Aidha katika mitandao ya kijamii  wa Twitter na Instagram, Nikki Wa Pili ametaja watu ambao wanaongoza kuangalia video chafu ambapo ameandika, "78% ya wanaotizama ngono mtandaoni ni wanaume, utazamaji huu unaleta uteja, wanachotizama ni vitendo vya kujamiana sio mapenzi wala mahusiano, tamaa ya kuhusiana inapungua, kusisimka kwa asili kuna potea, dhana ya ngono salama haipo ngono ya kawaida haiwasisimui.

Pia Nikki wa Pili ameendelea kuandika kuwa katika video za ngono vijana wanatazama aina ya wasichana kwa maana ya umbile, ukubwa na rangi.