"Nilikuwa najua ujauzito sio wangu" - Mabeste

Jumamosi , 23rd Mei , 2020

Msanii Mabeste ameshika tena vichwa vya habari vya burudani baada ya aliyekuwa mke wake kupata ujauzito na mwanaume mwingine ambaye alikuwa ni rafiki wa msanii huyo.

Kushoto pichani ni msanii Mabeste, kulia ni aliyekuwa mkewe Lisa akiwa na ujauzito wa mwanaume mwingine

Akizungumzia kuhusu ishu hiyo ya mzazi mwenziye kushika ujauzito na mwanaume mwingine kupitia show ya Friday Night Live ya East Africa TV, inayoruka kila siku ya Ijumaa kuanzia 3:00 hadi 5:00 usiku Mabeste ameeleza kuwa, 

"Kwenya maisha unapoishi unatakiwa utambue kwamba hii dunia kila mtu ana maono yake, kuna kitu unaweza ukaogopa kukifanya lakini kwangu inaweza ikawa nyepesi, kipindi kile tupo kwenye matatizo nilikuwa sijui kama anaujauzito ila nilikuwa nategemea, pia nilikuwa najua kama ujauzito sio wangu" amesema Mabeste 

Interview kamili tazama hapa chini.