"Nilikuwa naogopa baba au mama ataona" - Karen

Jumamosi , 4th Jul , 2020

Msanii Malkia Karen amefunguka kusema alikuwa anagopa yale yote aliyokuwa anafanya kwenye video ya wimbo wake mpya wakati wapo "location" wana-shoot video huku akihofia baba yake ataona.

Msanii wa BongoFleva Malkia Karen

Akizungumza kwenye show ya Friday Night Live Malkia Karen amesema, "Calisah ana unyama sana tena wa moto kabisa, kuna video za nyuma ya pazia zinakuja ndiyo unyama kabisa ila wakati tunashoot nilikuwa naogopaogopa sana nikawa nasema mbona tumesogeleana sana halafu kama baba yangu au mama ataona" amesema Malkia Karen

Zaidi tazama kwenye show kamili ya Friday Night Live ya East Africa TV.