Ijumaa , 30th Sep , 2022

Staa wa muziki nchini Kenya 254 Nyashinski ameahidi kufanya bonge la show siku ya Oktoba 1 pale Ware House Masaki kwenye jukwaa moja na Jay Melody na Ruger kutoka Nigeria.

Picha ya Nyashinski katikati akiwa na mtangazaji wa kipindi cha Drive Show Ian Dialo

Akizungumza na Drive Show ya East Africa Radio Nyashinski amesema "Ni mipango ya mungu tu, imekuwa muda mrefu kuja Dar kwenye show, lakini huu ndio muda sahihi kwa timu yangu na kwa mashabiki wangu. Itakuwa bonge la show".

Pia amesema mashabiki zake watarajie kusikia ngoma zake pendwa kama Now you know,Mungu pekee, Malaika, Sweet Aroma na Tuendelee ama tusiendelee akizipiga live.