Piere Likwidi atangaza kupunguza kunywa gambe

Jumatatu , 13th Jan , 2020

Mchekeshaji wa mitandaoni Piere Likwidi, amefunguka na kusema amepunguza unywaji wa bia na pombe kwa sababu sasa hivi anapokea tenda mbalimbali na mikataba ya kazi.

Picha ya Piere Likwidi

Piere Likwidi amefunguka hayo kupitia EATV & EA Radio Digital, ambapo amesema anaweza akafikisha hata wiki moja bila ya kutumia vinywaji vikali. 

"Nilivyokuwa nakunywa zamani na hivi sasa ni tofauti, kwa sababu sasa hivi nakuwa napata tenda mbalimbali na mikataba, kwahiyo siwezi kuwa nakunywa kama zamani nilivyokuwa najiachia kwa mfano asubuhi hadi asubuhi" amesema Piere Likwidi.

Aidha Piere Likwidi ameendelea kusema "Sasa hivi nakunywa kwa wakati naweza nikakaa hata wiki nzima nisinywe, navumilia tu nakunywa vinywaji baridi tu ni sawa" ameongeza.

Piere Likwidi amepata umaarufu mkubwa baada ya kuleta vituko vyake huku akiwa amelewa au anakunywa bia, na binafsi amekataa kuitwa jina la mlevi ila anataka aitwe mnywaji.