Jumanne , 22nd Jun , 2021

Msanii Recho Kizunguzungu amenyoosha maelezo ya stori ambazo zilikuwa zinasemekana kwamba anatumia madawa ya kulevya kwa kusema taarifa hizo zilimfanya kuachwa na Boyfriend wake na kukosa dili la kumuingizia pesa.

Msanii Recho Kizunguzungu

Akifunguka hilo kwenye show ya Planet Bongo ya East Africa Radio Recho Kizunguzungu ameeleza kuwa.

"Sijui kwanini watu walikuwa wanazusha kwamba natumia madawa, zile story zilisababisha watu waliokuwa wananisaidia waache kunisaidia, kuna dili nilikuwa nimelipata ila baada ya story hizo likapotea mpaka Boyfriend akaniacha alibaki Mama tu"

"Hiyo ishu ya madawa ilianza baada ya mimi kuwa karibu na mtu anayetumia, nakumbuka tulikuwa kwenye show Dodoma na TID, akapiga picha ya kawaida tu na mimi nilikuwa pembeni, so story zikaanzia hapo" ameongeza 

Msanii huyo kwa sasa amerudi baada ya ukimya wa miaka miwili na ameachia kazi yake mpya inayoitwa nikune.