
Kulia ni msanii Recho Kizunguzungu, kushoto Shilole
Akizungumzia hilo kupitia show ya DADAZ ya East Africa TV Recho anasema
"Kwenye suala la unene,kunenepa au kupungua ni mtu mwenyewe anavyotaka, Shilole anaishi mume wake na mumewe ameridhika mbona hajamwambia aende gym au aende China akajipunguze, ameridhika na mwanamke wake"
Recho Kizunguzungu ameongeza kusema kwamba hawezi kuishi maisha ambayo anapangiwa na watu bali anaishi anavyotaka yeye.