Rich Mavoko amerudi "Nimewa-miss watu wangu wote" 

Jumapili , 2nd Aug , 2020

Baada ya ukimya wa miezi nane bila kuachia ngoma mpya, kuonekana studio, kwenye interview, shughuli na hata mitandaoni, kwa mara ya kwanza msanii Rich Mavoko ametangaza kurudi kivingine kuzindua Minitape yake siku ya August 7.

Msanii wa BongoFleva Rich Mavoko

Mara ya mwisho Rich Mavoko kupost kwenye mtandao wa Instagram ilikuwa ni siku ya kusherekea Mwaka mpya wa 2020 yaani Januari 1, tangu hapo hakupost wala kushea kitu chochote hali iliyopelekea ukimya kutawala upande wake.

Ila kupitia ukurasa wake huohuo wa Instagram Rich Mavoko ametangaza kurudi kivingine baada ya kupost cover inayoashiria kuna tukio la kuzindua kazi zake siku ya August 7 katika hoteli moja Jijini Dar Es Salaam kisha akaandika.

"Nimewamiss watu wangu wote weka tarehe hii kichwani mwako, Rich Mavoko Minitape Launching" .