Jumapili , 9th Mar , 2014

Rapa Rich One anayewakilisha kundi mahiri la miondoko ya bongofleva nchini Wanaume Family ameibuka upya katika gemu na kuondoa fikra za watu kuwa amepotea katika fani na kwa sasa ameamua kujipanga kwa ajili ya kuachia project zake upya.

Kama ambavyo alivyoongea na eNewz Rich amesema anajipanga kama vile ujuavyo kumchinja kobe inahitaji timing, hivi sasa anafanya kazi zake akiwa solo na inapotokea kazi za kundi huwa anaungana nao kufanya kazi kwa pamoja.

Rich One amesema kuwa baada ya kufyatua trak na msanii Dully Sykes kilichobatizwa jina 'Apple La Kijani', mashabiki wake wategemee project zake mpya ambazo zitakuwa tayari kukamilika mwezi wa sita mwaka huu.