Msanii wa HipHop Roma Mkatoliki
"Nianze na neno samahani kama nitawakwaza watu lakini pia ninaweza nikawa na maana, lengo langu sio kuwadharau ama kuwavunjia heshima wasanii wa zamani, baadhi yao wanatuangusha sana wanapopewa 'mic' na kupanda jukwaani kufanya show, mnachokitoa hakiendani na matarajio ya mashabiki"
"Kumekuwa na malalamiko kwamba show wanapewa watu fulani lakini wengi wanaolalamika ni wasanii wa zamani kuwa hawapati nafasi lakini wanapopewa hawatumii vizuri hiyo nafasi kwanza wamesahau nyimbo zao, muda mwingi wanatumia kwenye kusema mikono juu" ameeleza Roma Mkatoliki
Zaidi tazama hapa chini kwenye video.







