Jumanne , 22nd Jun , 2021

Bosi wa Maybach Music Group (MMG) Rick Ross amethibitisha kuja na album mpya mwaka huu katika majira ya joto na ameiita ‘Richer Than I've Ever Been’.

Picha ya msanii Rick Ross

Kabla ya ujio wa album yake hiyo Rozay amesema ataachia ngoma mbili mfululizo wiki kadhaa zijazo kuanzia sasa.

Endapo atafanikiwa kuachia ‘Richer Than I've Ever Been’ basi itakuwa ni album ya 11 kwa Rozay baada ya  ‘Port of Miami’ ya mwezi Agosti 2019.