Alhamisi , 10th Oct , 2019

Baada ya kuwepo na taarifa nyingi zinazomhusu msanii  Lulu Diva kutelekeza mtoto, sasa leo Oktoba 10, 2019, ameweka wazi sababu zinazomfanya asitake kupata watoto kipindi hiki.

Msanii Lulu Diva

Lulu Diva amesema hayo baada ya kauli aliyoitoa msanii wa kundi la Navy Kenzo "Aika" ambaye alipost picha katika mtandao wa kijamii wa Instagram akisema, baadhi ya Wanawake wanahofia kupata watoto kwa sababu wanahisi wataharibu usichana wao.

EATV & EA Radio Digital imempata Lulu Diva, ambaye amesema kwa upande wake 'issue' ya kutotaka mtoto kwa sasa ni haijafikia muda sahihi wa yeye kuzaa, pamoja na kuwa na mambo mengi ya kufanya na kuogopa kulea.

"Mimi siogopi kuzaa kwa sababu ya nini, ila naogopa kuzaa sasa hivi kwa sababu sio muda sahihi kwangu na nina vitu vingi sana ambavyo nahitaji kuvitengeneza mimi mwenyewe, sitegemei kuzaa ili nimtegemee baba wa mtoto ambaye asipokuwepo mambo yaende hovyo, na mtoto anahitaji muda nahisi bado sijatulia kwa ajili ya kulea nahitaji muda zaidi" ameeleza.

Aidha ameeleza umri sahihi wa yeye kupata mtoto itakuwa miaka miwili au mitatu ijayo na mipango yake ni kupata watoto wanne hadi watano kwa kuwa kwao yeye amezaliwa peke yake hataki kupata mtoto mmoja pekee kwa sababu anajua itampa shida kwenye ukuaji wake. ameongeza.