Ijumaa , 10th Jan , 2020

Msanii wa filamu Aunty Ezekiel, amefunguka na kusema moja ya kitu ambacho kinafanya mahusiano yake kuvunjika ni usaliti, ambapo mpenzi wake akimfanyia hivyo basi mapenzi yataisha.

Msanii wa filamu Aunty Ezekiel

Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, Aunty Ezekiel, amesema kwenye mahusiano yoyote ambayo yanavunjika kila mtu huwa anakimbilia kusema yeye ndiyo amekosewa.

"Mahusiano yangu hayajawahi kuvunjika sana, tangu watu wamenifahamu yamevunjika mahusiano mangapi, ila mimi sipendagi usaliti, mtu akinisaliti mahusiano huwa siyawezi kabisa" amesema Aunty Ezekiel.

Aidha msanii huyo wa filamu ameendelea kusema "Unajua katika mahusiano yoyote ambayo utamuuliza mtu atakwambia yeye ndiyo amekosewa, lakini mimi naamini katika mapenzi watu hukoseana ila mimi sijawahi kumsaliti mtu".