Jumatatu , 3rd Oct , 2022

Msanii Nay Wa Mitego amepigia misumari kuhusu 'Title' yake ya kujiita jina la rais wa kitaa kwa kusema hata wananchi wanatambua kuwe yeye ndio msemaji wao na awawakilisha vyema.

Picha ya msanii Nay wa Mitego

"Mimi ni rais wa kweli wa kitaa. Wananchi wanatambua mimi ndio mwakilishi wao, msemaji wao na wanakubali. Unaweza ukaimba sana, ukatoa Hits song lakini mwisho wa siku jukwaani wanakupokeaje".

Nay wa Mitego amesema hayo kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio kila siku ya J3 mpaka Ijuma kuanzia saa 7:00 mchana mpaka saa 12:00 jioni.