"Sijapata ganda la ndizi au mteremko" - Q Chief

Jumanne , 13th Aug , 2019

Abubakar Shabaan Katwila maarufu kama Q Chief amefunguka kwa wale wote wanaomsema kuwa amepata mteremko kupewa gari na kutafuta kiki.

Akizungumza na EATV & EA Radio Digital, amesema kazi zake zilikuwa na nguvu kubwa kuliko gari alilopewa.

Gari ina thamani ya milioni 8 hadi 10, Video zangu tatu nilizotoa zina thamani ya milioni 20, muziki wangu auhitaji kiki kunirudisha wala vitu vingi ulikuwa unahitaji mtu mmoja ambaye ana uwezo wake binafsi ndio maana nililiaga hiyo kitu”, amesema.

Pia msanii huyo amewajibu wanaomsema amepata mteremko kupewa gari hilo kwa kusema alikuwa hajui kama atapewa gari na yeye sio mgeni wa gari kwa sababu alishamiliki magari matatu ila mambo yalimuendea tofauti.

Hata hivyo Q Chief ameendelea kusema gari huwa analitumia mpenzi wake, mama yake au meneja wake na ndoto zake ni kumiliki gari kubwa zaidi ya alilopewa.