
Mo Music
Akiongea na mwandishi wetu Mo Music amesema kuwa taarifa hizo hazina ukweli kwani hajawahi kushuka kimuziki na siku zote amejitahidi kukaa kwenye 'game' vizuri.
"Mimi sijawahi kushuka kimuziki, ninashukuru Mwenyezi Mungu kwamba ni mmoja kati ya wasanii ambao huwa wapo tu, haijalishi kitu gani kitakachotokea, tayari nimeshatengeneza msingi wangu kwa mashabiki na ninazidi kuwa mkubwa kila siku",alisema Mo Music.
Msikilize hapa akizungumzia suala hilo na kitendo cha kutoka kwenye uongozi wake wa zamani kwa ugomvi.