'Sikijui cheo cha Job Ndugai' - Shamsa Ford

Jumatatu , 2nd Dec , 2019

Msanii wa Filamu nchini Shamsa Ford, amesema kuwa hafahamu kama Mbunge wa Kongwa, jijini Dodoma Job Ndugai, kama ndiye Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Msanii wa Filamu nchini Shamsa Ford.

Shamsa Forda ametoa kauli hiyo wakati wa mahojiano kwenye kipindi cha KIKAANGONI, kinachorushwa kila siku ya Jumatano kupitia kurasa za Facebook na YouTube ya East Africa TV, alipotakiwa kutaja vyeo vya baadhi ya viongozi wa Kitaifa na ndipo alipopatwa na kigugumizi kutaja cheo Mheshimiwa Ndugai.

"Mimi najua Samia Suluh ni Makamu wa Rais , Majaliwa ni Waziri Mkuu, Job Ndugai sijui cheo chake ni kipi" amesema Shamsa Ford.

Tazama video kamili hapo chini dakika 51:27