Jumamosi , 12th Oct , 2019

Msanii wa BongoFleva nchini, Hawa ameonekana kujutia kitendo cha kukaa nje ya muziki kwa muda mrefu, wakati anasumbuliwa na matatizo ya afya, ambapo amesema kwasasa muziki umekuwa kama vita.

Picha ya msanii Hawa Ntarejea

Hawa Ntarejea ameeleza hayo kwenye kipindi cha Friday Night Live "FNL" ya EATV, wakati anatambulisha video ya wimbo wake mpya uitwao Shagala bagala.

"Naona muziki ni vita nina muda mwingi sana nimepoteza kutokuwa kwenye 'game', mimi naamini kila mtu ana kitu chake, halafu shabiki zangu lazima nitakuwa nao na sifanyi kwa sababu wengine wanafanya, nisije nikavunjika moyo moja kwa moja maana kila mtu ana nafasi yake" amesema Hawa.

Hawa ameendelea kusema, watu wasitarajie kumuona akirudi kwenye masuala ya utumiaji wa pombe na madawa ya kulevya kwa sababu ameshajiahidi yeye mwenyewe, kwamba shetani asimsogelee na asirudi kule alipotoka maana atapotea. 

Aidha Hawa amesema kuwa huenda asingepitia  matatizo, sasa hivi angekuwa mbali ila anamshukuru Mungu kwa mapito ambayo yamemtokea na anaamini kuna mambo mengine ameyaepuka kutokana na aliyopitia, hata mama yake sasa hivi amependeza na kunawiri sio kama zamani, alivyokuwa na mawazo wakati anasumbuliwa na maradhi.