
Nyauloso ameyasema hayo alipokuwa kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, na kusema kuwa ingawa anapata fursa za kutengeneza skendo, lakini yeye haishi kwa kutegemea kiki.
“Oportunity ipo ila sipendi iwe hivyo, sipendi kudate na mtu maarufu nahisi career yangu ya muziki sijapanga niitengeneze hivyo, sipendi kudate na mtu maarufu , awe muimbaji au muigizaji, labda naweza nikatoka na mtangazaji”, alisema Nyauloso
Pia Nyauloso amesema licha ya muziki yeye ni mfanyabiashara, hivyo ana uwezo wa kuingiza pesa za kutosha, na hivyo kufanya kuwa na mtaji wa kutosha kuwekeza kwenye muziki.