
Snura na Shilole.
Snura amefunguka hayo wakati akizungumza na www.eatv.tv, ambapo amesema kuwa Shilole na yeye walikuwa na mpango wa kufanya kazi wakati ule ili kuonesha kuwa hawakuwa na tofauti lakini muda ulikosekana.
"Uhusiano wangu na Shilole haujawahi badilika, upo vilevile tangu tulipozaliwa na umesimama palepale kama picha la 'bisimini'", amesema Snura.
Akizungumzia mafanikio yake katika sanaa, Snura amesema kuwa anajivunia vitu vingi ambavyo amevipata kupitia muziki lakini hapendi kuonesha.
"Nina vitu vingi vya kujivunia lakini siwezi kunadi mali zangu mtandaoni, mimi huwa na nadi kazi tu", amesema Snura.
Bofya link hapo chini kumtazama Snura akifunguka zaidi.