Jumatano , 14th Dec , 2016

Mwanamuziki Spicy kutoka Nigeria ambaye pia ni mpenzi mpya wa Lady Jaydee, leo ametoa sababu za wawili hao kutokuwa na pete licha ya kuonekana wakiwa katika mazingira walioyaita 'honeymoon'.

Spicy (Kushoto) akiwa na Jay Dee ndani ya Planet Bongo EA Radio

 

Akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, Spicy amesema kwa sasa anasubiri hatua za uchumba na ndoa zikamilike, kisha ndipo suala la pete litafuata.

"The ring is coming after the engagement and the wedding, we don't start with the ring....akimaanisha (Pete itakuja baada ya uchumba na ndoa, hatuanzi mahusiano na pete".

Kwa sasa msanii huyo yupo nchini na wameachia kazi mpya ya pamoja akiwa na Lady Jaydee.

Tazama video hapa chini akijibu suala la pete huku Lady Jaydee akifurahia.