Jumanne , 24th Mei , 2022

Mzee wa commercial AY ametoa credit zake kwa msanii Joseph Mbilinyi Mr II Sugu baada ya kusema amewa-inspire sana kufanya mziki na vitu vingine.

Picha ya AY kushoto na Mr II Sugu kulia

"Nafurahi sana kuwa kwenye tukio hili la kihistoria, kiukweli Sugu ametu-inspire sana hata mimi binafsi tangu naanza kutoa wimbo wa kwanza mpaka leo hii ametu-inspire kwa vitu vingi"

"Katika nyota zake alizoziweka kuanzia alivyokuwa mlinzi na kuuza mitumba alisahau kwenye upande wa siasa, yeye ndio msanii aliyeingia kwenye siasa akawa mheshimiwa na ilifungua njia kwa watu wengine ambao walikuja baadaye" ameeleza AY