Surprise ya Rais wa BongoFleva, akabidhiwa gari

Jumatatu , 13th Jul , 2020

Leo ni siku mpya ya historia kwa wapenzi wa burudani, baada ya mtangazaji wa kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio na Rais wa BongoFleva kwa sasa Dullah Planet, kuahidi ushindi kwenye burudani ya muziki.

Rais wa BongoFleva na mtangazaji wa kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio akikabidhiwa gari mpya aina ya Mercedes Benz

Akizungumiza hilo baada ya kuzinduliwa kwa kampeni ya #SimamaNaMimi Rais wa BongoFleva Dullah Planet amesema, wanahitaji vitu vidogo kama kumaliza bifu za wasanii, upendo na umoja ili kuweza kushindana na wakali wa muziki kama Nigeria ambao wanafanya vizuri kwa Bara la Africa.

Aidha mtangazaji huyo amefanyiwa surprise ya gari jipya aina ya Mercedes Benz, ambapo mwenyewe amesema "Nikisema sijashtuka nitakuwa muongo, ni kitu kizuri na nastahili hili kwa sababu nimekuwa hapa kwa miaka 12, nina haki ya kupata kwa mengi ambayo nimeyafanya hapa East Africa Tv na Radio na ni motisha ya kufanya makubwa".