T Touch azungumzia Young Dee kulelewa Marekani

Jumatano , 21st Aug , 2019

'Producer' mkali wa muziki wa Bongo Fleva, Mr T Touch amezungumzia juu ya tetesi kuwa msanii Young Dee kutunzwa na mwanamke aliyemzidi umri huko nchini Marekani.

Young Dee na mpenzi wake

Akipiga stori na eNewz, T Touch amesema kuwa sio jambo la kushangaza kuona suala hilo kwani watu wengi wanasafiri nje na hawazungumzwi, huku akisisitiza kuwa amekwenda kufanya maisha yake.

"Mbona kawaida hiyo?, watu wengi tu wanasafiri nje kila siku. Young Dee ni mtoto wa kiume amekwenda kutafuta maisha yake mwenyewe na sio lazima afikie kwa mtu ambaye mtamfahamu", amesema T Touch.

"Hakuna mama ambaye anamlea Young Dee, ni 'husling' zake tu za maisha watu wasilazimishe", ameongeza.

Young Dee ambaye yupo chini ya 'production' ya Mr. T Touch, hivi sasa yupo nchini Marekani takribani mwezi mmoja, ambapo amekuwa akionekana mtandaoni mara kadhaa na mwanamke anayeonekana kumzidi mwili na umri.

Mtanzame T Touch akizungumza zaidi hapa.