Tunda na Whozu wameachana? Mpenzi wa Tunda ni huyu

Jumamosi , 11th Jan , 2020

Wiki iliyoisha kulisambaa taarifa ya kuachana kwa video vixen Tunda pamoja na mpenzi wake Whozu, sasa hilo huenda jambo hilo likawa limetimia.

.Tunda na mpenzi wake mpya

 

Kupitia katika mtandao wa Instagram, ukurasa wa Tunda amepost picha ya mpenzi wake mpya aitwaye Otike raia wa Nigeria, ambaye anasadikika kuwa naye kwenye mahusiano kwa sasa kisha akaweka alama ya kopa na kuandika "Povu ruksa".

Baada ya muda mfupi Tunda kupost picha hiyo Otike mwenyewe alikuja ku-comment kwenye picha hiyo kwa kuandika "Nakupenda my Princess".

Penzi la Tunda na Whozu limedumu kwa muda wa mwaka mmoja, na katika historia inaonyesha Whozu ndiyo mwanaume ambaye ameweza kukaa na Tunda kwa muda mrefu zaidi kwenye mahusiano.