Tundaman atoa sababu ya ugomvi wake na Matonya

Alhamisi , 11th Jul , 2019

Kapteni wa muziki wa Bongo Fleva Tundaman, amefunguka sababu za yeye kutokuwa na maelewano na msanii mwenzake Seif Shabani, maarufu kama Matonya.

Tundaman

Tundaman amesema hayo leo kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, na ameeleza chanzo cha wawili hao kuwa na tofauti ni Matonya kumuiga sauti yake.

"Wakati nakutana na Matonya alikuwa na ngoma mbili tu, baada ya kukutana na mimi ndio nikampa madini ya tone ya sauti yangu, yeye ndio ananiiga mimi sauti. Nakumbuka kipindi kile alikuwa anakaa Kariakoo akawa mshikaji wangu sana, tulitaka kuanzisha kundi na nilimmezesha ngoma nyingi na nilimuandikia ngoma, ana material yangu mengi".

Aidha Tundaman amesema hajawahi kusikiliza nyimbo za Dogo Janja, na jana ndio ilikua mara ya kwanza kusikiliza baada ya kiugundua kuwa wametumia neno moja la "Kibada" kwenye ngoma zao.