Vanessa afunguka kikwazo cha ndoa na Jux

Alhamisi , 18th Apr , 2019

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee ambaye kwa muda mrefu amekuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na msanii mwenzake Juma Jux, amefunguka kitu kinachowapa ugumu wawili hao kufikia hatua ya kufunga ndoa rasmi.

Akizungumzia hilo Vanessa Mdee amesema kwamba watu wote wanajua kuwa yeye ni Mkristu na Jux ni Muislamu, na ndiyo changamoto kubwa wanayokabiliana nayo.

Vanessa afunguka zaidi 

“Ndoa ni jambo la baraka sana ndoa ni next step to everyone ambaye amekuwa kwenye mahusiano kwa muda mrefu, lakini ni wazi kuwa Juma ni Muislamu na mimi ni Mkristu, nadhani watu wengi wana hiki kitu, muda mwengine inaleta changamoto sana”, amesema Vanessa.

Hata hivyo Vanessa amekanusha tuhuma za penzi lao kufa (kuachana) na kusema kwamba bado wapo pamoja na bado anampenda sana Jux.