Vanessa Mdee amjibu Madee na Nandy

Ijumaa , 9th Aug , 2019

Vanessa Mdee "Vee Money"amejibu alichoandika msanii Madee baada ya kuona hakuna hata msanii mmoja wa HipHop kutokea Tanzania katika tuzo za Afrimma.

Akizungumza na EATV & EA Radio Digital, Vanessa Mdee ameeleza kuwa,

"Hili suala limenipa tatizo na ninajiuliza, kwa sababu hata mimi najihusisha na familia ya HipHop, nahisi kuna tatizo lakini silifahamu kwa sababu kwenye upande wa sanaa vipaji vipo muziki mzuri upo wanajitangaza vizuri labda tatizo ni nidhamu ya usanii".

Kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter, Madee ameandika kuwa aliwahi kusema kwamba HipHop haiuzi ila kuna wapuuzi walimpinga, akiangalia tuzo za Afrimma haoni hata msanii mmoja wa HipHop kwa mwaka wa 5 sasa.

Aidha msanii huyo ameongelea suala la kutokuwepo kwenye tamasha la Nandy Festival kwa kusema alikuwa nchini Ureno na anampongeza sana kwa kufanya kitu kikali.