Jumanne , 13th Mei , 2025

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Vanillah kutoka label ya muziki ya Kings inayomilikiwa na msanii Alikiba amefunguka mpango wake wa kuondoka katika label yake hiyo.

 

Mbali na hilo pia Vanillah ameeleza pia kwa nafasi yake kuhusu kile kinachoendelea kwa msanii mwenzie Ibraah kutoka Record label ya Konde Gang ambaye ametangaza kuondoka katika label hiyo ambapo ameomba kuchangiwa na wadau ili aweze kulipa pesa ya kuvunja mkataba wake ambayo ni Bilioni moja za kitanzania

"Mimi kitu ambacho napambana nacho kwasasa ni kuhakikisha napambania muziki wangu sana kwasasa nikiwa bado kings na ninafurahia kabisa kuwa chini ya label ya Kings (Record label ya msanii Alikiba) '' Ameeleza Vanillah

"Kuhusu rafiki yangu Ibraah ambao wameona akiomba wamchangie niwaombe tu kuwa mumsikilize na mufuate kile ambacho anakiongea kwasababu kile ndio ambacho kipo kwa wakati huu,kuhusu kumchangia na mimi nimemchangia" Ameeleza Vanillah